Kilichomfanya kocha asimpange MO Salah

Muktasari:

Hisia za uchovu huweza kuhisiwa zaidi katika maeneo ya maungio (joint), mgongoni, kiunoni, mapajani na magotini.

Uchovu unasababisha misuli ya mwili kukosa nguvu kama ilivyo kawaida yake. Tatizo hili linaweza kuambatana na maumivu yanayoweza kuwa ya wastani mpaka kuwa makali.

Hisia za uchovu huweza kuhisiwa zaidi katika maeneo ya maungio (joint), mgongoni, kiunoni, mapajani na magotini.

Katika mechi yapili ya ufunguzi la kundi A katika mechi ya Misri na Uruguayi shauku kubwa ilikuwa ni kumwona staa wa misri Mohamed Salah akicheza lakini kwa bahati mbaya hukupangwa.

Itakumbukwa kuwa kabla ya michuano hiyo kuanza alipata majeraha ya kuteguka bega na kujeruhi tishu laini wakati wa fainali ya UEFA mwishoni mwa mwezi wa jana.

Pamoja na kuwa majeruhi alijumuishwa katika timu ya taifa lakini alikuwa bechi katika mechi yapili ya ufunguzi iliyochezwa siku ya ijumaa.

Salah hakupangwa kwasababu bado ana maumivu katika ungio la bega ambayo yanatoa ishara kuwa inahitajika muda zaidi kuweza kupona, kitabibu sio sahihi mchezaji kuchezeshwa akiwa na maumivu.

Kwa kutumia tukio la Salah nitawapa ufahamu ili kuwapa uelewa kuepuka kucheza ukiwa na maumivu au kabla ya jeraha kupona.

Kucheza mchezo ukiwa na maumivu kunaongeza ukubwa wa tatizo kwani jeraha linapotoneswa mara kwa mara ni chanzo cha kujijeruhi upya na hivyo kuchelewa kupona.

Maumivu kwa mwanamichezo aliye majeruhi ni ishara kuwa jeraha bado halijapona vizuri.

Maumivu yanaweza kuwa ya kawaida, ya kati na makali. Yanaweza kuwa ni majeraha ya mfupa, misuli, mishipa ya fahamu na tishu nyingine za mwilini.

Panapotokea jeraha mwili hujibu mapigo kwa kutuma askari mwili kwa ajili ya kukarabati neneo hilo.

Mlipuko wa kinga ya mwili ndio chanzo cha mtu kuhisi maumivu, kufa ganzi, kuvimba, kupata joto na kubadilika rangi ya ngozi. Hali hii ndio kitabibu huitwa inflammation.

Wanamichezo ambao wako nje ya uwanja kwa kuwa majeruhi hudhani kuwa maumivu yanapopungua tu wamepona na wako fiti kuanza kucheza pasipo kufahamu kuwa jeraha bado halijapona vizuri.

Mara yingine misuli ya mwili ya mwanamichezo inapotumika sana huambatana na vimichubuko vya ndani kwa ndani ambavyo uwapo wa maumivu ni kama ombi la mwili kuhitaji kupumzika ili kupona kabisa.

Unapobainika na wataalam wa tiba za michezo kuwa una majeraha ya mfupa na nyuzi ngumu (tendon na ligaments) fahamu kuwa itachukua muda kupona kabisa na kurudi mchezoni.

Mwanamichezo anahitajika kujifahamu na kujidhibiti binafsi na maumivu yake ikiwamo kujua yanachokozwa na mambo gani, je yanaanzaje wakati wakuanza, katikati au mwishoni baada ya mazoezi au mchezo?

Vile vile kufahamu kuwa maumivu yanauma unapominywa au yanakuwepo tu yenyewe, je yanasambaa au yanaibukia sehemu nyingine.