#WC2018: Kumbe Uwanja wa Ekaterinburg Arena umetobolewa bana!

Muktasari:

  • Uwanja huo sasa una uwezo wa kuchukua mashabiki 35,696 na ujenzi wake ulikamilika Machi 2018. Mara ya kwanza ulijengwa mwaka 1957 na umegharimu Dola215m

Kwa walioko Russia, kila atakayesogelea Uwanja wa Ekaterinburg Arena hawezi kuacha kushangaa jinsi ulivyoandaliwa kwa fainali hizo.

Uwanja huo sasa una uwezo wa kuchukua mashabiki 35,696 na ujenzi wake ulikamilika Machi 2018. Mara ya kwanza ulijengwa mwaka 1957 na umegharimu Dola215m

Mechi ambazo zimechezwa kwenye Uwanja huo zilikuwa za Misri na Uruguay; Ufaransa na Peru, Japan na Senegal, mechi ya Mexico na Sweden ya Juni 27.

Uwanja huo umejengwa kisasa kama ulivyo Luzhniki, umedizainiwa vizuri ukiwa unang’aa na kinachovutia ni jinsi ulivyojengwa kwa nje. .

Ekaterinburg Arena umejengwa ili kukidhi mahitaji ya mnashabiki 35,000 kiwango kinachotakiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa.

Jukwaa hilo limejengwa kwa kutoboa uwanja na liko kwa nje ili kuongeza idadi ya mashabiki kwani kabla ya kufikia 35,000 ulikuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 23,000.

Ekaterinburg Arena, kati ya viwnaja vya Fainali za Kombe la Dunia 2018 unacheklesha kwani unalipa, unaingia ndani halafu unakwenda kukaa nje ya uwanja.

Mashabiki wa Misri na Uruguay walilazimika kushangilia timu zao wakiwa nje ya uwanja lakini majukwaani.

Why not build two temporary, 45-metre stands outside the venue and offer the fans a view through big holes at either end of the ground?

Hata wakaguzi wa viwanja kutoka Fifa walibaki kushangaa walipofika kwenye

Ekaterinburg Arena na zaidi walikuwa wakijitafakari suala la usalama wa mashabiki.”

Wahandisi wa Russia waliwaeleza kuwa utaalamu huo ni mahsusi kwani jukwaa linajengwa kwa muda maalumu na baadaye linaondolewa na jukwaa kuzibwa.

Fainali zitakapomalizika, litang’olewa na uwanja utasalia na mashabiki wake walewale 23,000 wa uwanja huo unaotumiwa na klabu ya FC Ural Yekaterinburg.