Mbegu hizi si za kukosa wakulima wa maharage

Manufaa ya vituo vya utafiti wa kilimo ni pale vinapowasaidia wakulima kufanya uzalishaji wa kisasa na wenye tija.

hiki ndicho kilichofanywa na kituo cha utafiti cha Selian(SARI) kilichopo jijini Arusha, baada ya kugundua aina tisa mpya za mbegu za maharage.

Ni mbegu ambazo kwa mujibu wa watafiti wa kituo hicho zina uwezo wa kuvumulia ukame, kuzaa zaidi na hivyo kuwa na soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Mbegu hizo ni Selian 9, Selian 10, Selian 11, Selian 12, Selian 13, Selian 14, Selian 15, Uyole 17 na Uyole 18.^Maharage ya kusindika^Mtafiti John Msaki, anasema kati ya aina hizo tisa, aina

tatu ambazo ni Selian 9, Selian 10 na Selian 11 ni kwa ajili ya usindikaji.

‘’Kwa mara ya kwanza tumeweza kuwa na maharage ya kusindikwa, kwani maharage hayo yalikuwa yakiagizwa kutoka nje ya nchi. Kwa sasa hivi tumevuka hatua na

yatapatikana hapahapa Tanzania,’’ anasema.^Anasema kuwa, maharage hayo ni kwa ajili ya chakula na yanaokoa muda, kutokana na kutotumia muda mwingi wakati wa kuyachemsha.^Anasema kuwa, maharage hayo ya usindikaji yalianza kufanyiwa utafiti katika kituo hicho mwaka 2015, kwa ajili ya kuangalia kama yatawafaa wakulima pamoja na kuangalia uzalishaji wake, Ndipo walipogundua kuwa yana uwezo wa kuzalisha zaidi.^‘‘Hapa nchini hatujawahi kuwa na maharage ya kusindikwa ambayo yanalimwa kwa siku 90 tu,’’ anaeleza.^Selian 14 na 15

Mtafiti Mary Mdachi, anasema maharage aina ya Selian 14 na Selian 15 yana utajiri wa madini ya chuma na zinki.^Anasema kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania inaungana na nchi nyingine katika ukanda wa Maziwa Makuu ambazo zimeshatoa aina hizo za maharage. Anazitaja nchi hizo kuwa ni Rwanda, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Uganda.

Anasema aina hizo zimegunduliwa kutokakana na msukumo wa kupambana na tatizo la utapiamlo kwa

kwa watoto chini ya miaka mitano na wanawake walio kwenye umri wa kuzaa.^‘’Maharage hayo yanasaidia kuongeza kiwango kikubwa cha damu mwilini, huku madini ya chuma yakisaidia ubongo kufanya kazi na kuondoa msongo wa mawazo,’’ anasema na kuongeza:^‘’Maharage hayo yanaongeza chembechembe

nyekundu za damu ambazo ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa ubongo, uwezo wa kuelewa, mfumo wa fahamu na uzazi na pia kupunguza udumavu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.’’^Aidha, anasema mbegu hizo zina uwezo wa kulimwa katika eneo dogo, kwani yana uwezo wa kutambaa kwenye miti.^Selian 12, Selian 13, Uyole 17 na yole 18 ^Kwa mujibu wa mtafiti wa magonjwa ya mimea katika kituo hicho, Edith Kadege, aina hizi zinavumilia ukame

kwa kiasi kikubwa, huku yakikomaa ndani ya siku 65. Pia, anasema yanaweza kulimwa katika maeneo yasiyokuwa na mvua za kutosha.^Mkulima Elly Nanyaro anasema mbegu hizo zitawasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji na hatimaye mapato, huku akiomba watafiti waharakishe kuziingiza aina sokoni aina hizo za mbegu.^Agizo la Waziri

Akizindua mbegu hizo, Waziri wa kilimo Charles Tizeba, alitoa agizo kwa watafiti kuhakikisha mbegu hizo zinazalishwa kwa wingi na mwishowe kuwafikia wakulima kwa wakati hususani katika msimu wa kilimo.