Siasa zetu zilenge kujenga EAC, AU ikiwamo kuupinga ubaguzi

Katika makala iliyopita tulijadili siasa zetu na wazo zima la uzawa. Makala yenyewe haikulenga kupigia debe ubaguzi kwa kuwa uzawa na ubaguzi ni vitu viwili tofauti.

Katika taifa letu tunaendelea na zoezi la kuwafukuza wahamiaji haramu ili kulinda usalama wa nchi na watu wake. Ingawa lengo ni zuri, wasiwasi ni utekelezaji wake ambao unaweza kuwa chanzo cha ubaguzi, chuki na uonevu.

Wakati tunaendelea na mjadala wa kuziunganisha nchi za Afrika ya Mashariki na Afrika nzima, tunaendesha zoezi la kuwafukuza watu kutoka kwetu, tunataka kuishi kama kisiwa?

Watu wetu wa Afrika wametengwa kwenye mipaka ya kutengenezwa, ambayo iliwatenga ndugu, koo na makabila. Mfano kuna ukoo ambao watu wake wako Uganda wengine Tanzania. Vivyo hivyo kuna makabila ambayo yako nchi tatu tofauti. Uganda, sehemu nyingine iko Rwanda na sehemu nyingine Burundi. Katika hali kama hii ni lazima tuwe na hekima na busara.

Tujenge mazingira ya kuishi na watu ambao tuko wamoja, lakini tunatengwa na mipaka ya kutengenezwa na watu. Hapa tunahitaji wanasiasa wanaoongozwa na hekima na busara. Ndiyo maana Mwalimu Nyerere, alisema ili tuendelee tunahitaji siasa safi. Hii ni siasa ya wetu wenye hekima na busara.

Wanaumajumuhi wa Afrika kama akina Kwame Nkrumah, waliguswa na ubaguzi wa mtu mweusi. Waliguswa na nyanyasaji, kupuuzwa na unyonge aliokuwa akilazimishwa kuishi mtu mweusi nje na ndani ya Afrika.

Nkrumah alipokwenda kusoma nje, ubaguzi aliokumbana nao ulimlazimisha kufikiria na kupanga mkakati wa kumkomboa mtu mweusi na kuhakikisha weusi wanaungana kupambana na wakoloni.

Mbali na Waafrika waliokuwa wakienda Ulaya na Amerika kusoma, kuna watu weusi waliopelekwa huko utumwani. Hawa nao walichukia ubaguzi na kuamua kuunda umoja wao wa kuunganisha Afrika. Weusi kutoka Afrika, waliokuwa wamekwenda kusoma walihimizwa kurudi nyumbani kuzikomboa nchi zao kutoka mikononi mwa wakoloni. Na wale waliokuwa huko nje (Diaspora) walitakiwa wapambane kurudisha heshima ya mtu mweusi na hatimaye kuwaunganisha watu weusi popote walipo chini ya msingi wa Bara lao la Afrika, yaani ‘Umajumuihi wa Afrika’.

Tukiweza kutumia DNA, na sisi hapa Afrika tunaweza kugundua jinsi tulivyo wamoja. Tunaweza kujikuta ni familia moja. Mtu wa Sudan, anaweza kuwa na jamaa zake Zambia, DRC au Afrika ya Kusini. Kabla ya mipaka ya kikoloni, Waafrika walikuwa wakihama kutoka eneo moja hadi jingine. Hivyo jitihada za kujenga daraja la “Diaspora” na Afrika, ziende sambamba na kujenga daraja la kuunganisha “Diaspora” ndani ya Afrika. Tuache kubaguana kwa kuangalia pua zetu, rangi zetu na lugha zetu. Tukubali kwamba binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja na ni lazima Afrika iungane. Nyerere, alichukia ubaguzi. Alisema ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu. Kwamba mtu akishaonja nyama ya mtu hawezi kuacha.

Padri Privatus Karugendo

+255 754 633122

Dhambi hii ya ubaguzi ikishaingia kwenye roho ya mtu kutoka ni shida.

Aliuchukia ubaguzi na alipambana nao ndani ya nchi na nje ya nchi. Tanzania ilikuwa kimbilio la kila mwanadamu. Wapigania uhuru waliweka makambi yao hapa na kuishi kama Watanzania. Wakimbizi walipokelewa kutoka kila pembe ya Afrika, na kuishi kama Watanzania.

Hospitali za makanisa mkoani Kagera zimewapoteza waganga na wakunga wangapi kwa sababu hizohizo?

Lakini wakati wa zoezi la kuwafukuza wahamiaji haramu; tumewafukuza walimu, madaktari na wataalamu wengi. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kiliwapoteza wataalamu wangapi waliondoka na kurudi Rwanda, kwa vile walikuwa wananyooshewa kidole cha uhamiaji haramu?

Hospitali za makanisa mkoani Kagera zimewapoteza waganga na wakunga wangapi kwa sababu hizohizo? Tuache ubaguzi na kukumbatia hoja ya umajumuhi wa Afrika. Tunahitaji siasa safi, siasa zinazoongozwa na hekima na busara.

Padri Privatus Karugendo

+255 754 633122