Uhuru ataka uchunguzi mali za vigogo uanze kwake, Ruto

Muktasari:

  • Matamshi ya Uhuru yamewapa matumaini Wakenya wengi kwamba vita dhidi ya ufisadi sasa vinaweza kuzaa matunda.

“Mali zangu zitapelelezwa kisha za Makamu wa Rais na hatimaye mawaziri, magavana, mawaziri na wengine,” anasema Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta baada ya kuzika tofauti zake na Gavana wa Jimbo la Mombasa Hassan Joho.

Matamshi ya Uhuru yamewapa matumaini Wakenya wengi kwamba vita dhidi ya ufisadi sasa vinaweza kuzaa matunda.

Lakini mbali na hayo, baadhi ya Wakenya wana wasiwasi, wanadai kwamba vita hivyo haviwezi kwenda popote kwa sababu viongozi wote wa kisiasa ni wezi tangia zamani.

Hata hivyo, tangazo hilo limewatia kiwewe baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa umma ambao utajiri wao hauelezeki kwa sababu unatokana na wizi wa mali za umma.

Mitandao ya kijamii nchini Kenya imesheheni mazungumzo na mijadala kuhusu tangazo hilo la Rais alilolitoa akiwa ziarani Mombasa.

Kupitia mitandao hiyo, wananchi ‘wanamsaidia’ Rais na maofisa wa jinai kujua mali ya viongozi mbalimbali.

Katika mijadala hii haswa katika Twitter, Wakenya wanaorodhesha baadhi ya viongozi ambao wamekuwa mabwanyenye kwa muda mfupi baada ya kuanza kuwa watumishi wa umma.

Baadhi yao wametajwa kwa kuhamia mitaa ya kifahari ghafla ilhali wamekuwa wakiishi uswahilini kwa muda mrefu.

Mathalan, wanamtaja mwanasiasa mmoja wa ngazi za juu katika serikali ambaye ameupa mkono wa buriani ufukara uliokuwa umemwandama kwa miaka mingi hadi alipoanza kutumikia umma katika nyadhifa mbalimbali.

Mwanasiasa huyo ana helkopta saba za kisasa anazokodisha kwa serikali na kampuni za serikali kila siku.

Serikali humlipa Ksh230, 000 (Sh5,060,000) kwa saa moja kukodisha ndege hizo. Bila shaka huku Wakenya wakinyeshewa na mvua, mwanasiasa huyo hunyeshewa pesa.

Katibu mkuu mmoja serikalini yasemekana alinunua malori matano mapya kutoka katika kampuni moja inayouza magari kutoka ng’ambo. Pia, Katibu huyo alinunua ekari 38 za ardhi kwa Ksh3 milioni (Sh66 milioni) kwa ekari moja. Je, alipata wapi pesa hizi zote. Isitoshe, alinunua nyumba zipatazo tatu za kifahari ilhali mshahara wake hauwezi kumruhusu kuwa na mamilioni ya pesa.

Vita inamlenga Ruto?

Ingawa juhudi za kupambana na visa vya ufisadi ambavyo wengine huita mlungula, chai au kitu kidogo, kuna viongozi wanaokejeli msimamo wa Rais Uhuru.

Tangu Rais atangaze vita dhidi ya janga hili la ufisadi, chama cha Jubilee kimepasuka mara mbili; kuna upande wa Uhuru na mwingine wa Ruto. Ni upande wa Ruto unaolia mno juu ya mipango ya kupunguza ama kuzika kabisa ufisadi.

Wanadai juhudi za Rais zinamlenga Ruto na marafiki wake wa kisiasa ili kudidimiza ndoto yake ya kutaka kuwa rais 2022.

Mrengo wa Ruto unataka tathimini ya mali ya viongozi na watumishi wengine ipanuliwe ili viongozi wa kuanzia 1963 pia wachunguzwe ili ibainike walipataje utajiri wao.

Mbunge mmoja ambaye ni jirani na rafiki wa Ruto anapendekeza kwamba tathimini ya mali na maisha ya viongozi na watumishi ianzie mwanzilishi wa taifa la Kenya, Mzee Jomo Kenyatta ambaye pia ni babake Rais Uhuru.

Kauli kama hizo bila shaka zinakejeli na kufanyia mzaha juhudi za kupambana na adui huyu wa maendeleo. Pia, ni kama kambi ya Ruto haielewi kwamba mambo yamebadilika na hivi karibuni baadhi yao watajuta kupora mali ya walipa kodi.

Wanasiasa na baadhi ya mafisadi hawajawahi kuchukulia vita hivi kwa umakini; wanadhani kuwa ni mchezo; hawajui wakati huu kumekucha na wanaolengwa afadhali wajitayarishe kukutana na mkono mrefu wa sheria.

Sababu za kujilundikia pesa

Wanasiasa hutumia mamilioni ya pesa katika kampeni za kusaka kura na wanapochaguliwa huwa wanatafuta njia zozote za kurudisha pesa walizotumia wakati wa kampeni.

Vilevile, wanazingirwa na tamaa ya kujilimbikizia mali ili waweze kufanya kampeni ya uchaguzi mkuu unaofuata bila matatizo ya kifedha.

Aidha, pia huwahonga wapinzani wao na wafuasi ili wasiwe na wakati mgumu. Hizi ni baadhi ya sababu ambazo inapalilia ufisadi .

Lakini, ingawa baadhi ya viongozi wa Kenya hawaamini kwamba ni wakati wa kupigana na ufisadi, kuna wengine wanaoamini.

Somo hadi nje ya nchi

Wiki jana, Wakenya waliingia kwenye mitandao ya kijamii kuwakejeli na kuwasuta wabunge wanane kutoka Zambia waliozuru nchini kwa minajili ya kuona jinsi Kenya inavyopigana na ufisadi.

Wengi walisema wabunge hao wanafanya mzaha na wamekuja kujifunza njia na mbinu mpya za kupora walipaji kodi wa nchi yao.

Walipowasili, wabunge hao walikwenda moja kwa moja hadi makao makuu ya Tume ya Kupambana na Ufisadi nchini (EACC) na kufanya kikao cha muda na makamishna wa tume hiyo.

Wakenya walicheka huku mbavu zikawauma baada ya kupokea habari hizo. Wananchi wanasisitiza kwamba, Kenya si kielelezo kizuri cha nchi inayopigana na ufisadi.

“Kile tunachoweza kuwafunza Wazambia ni jinsi ya kuiba na kufanikiwa kama mafisadi Wakenya. Wapenzi Wazambia, hakuna tofauti kati yenu na sisi,” akasema mtumiaji wa Twitter anayejulikana kama @Jma.

“Nasikia wabunge wa Zambia wako hapa kujifunza mikakati ya kumenyana na visa vya ufisadi! Tafadhali, mtazame mawingu, huenda ikanyesha leo,” akasema Jenaro Wachira kwenye Twitter.

@Vikiyo aliandika, “Wabunge hao hawana budi kunaswa na kuwekwa ndani kwa sababu ya kutumia vibaya mali ya umma. Hapa Kenya tunafunza tu jinsi ya kuharakisha ufisadi. Sisi ndio wenyewe.”

“Nini mbaya na Serikali ya Zambia! Siamini iliwatuma wabunge wake hapa kujifunza jinsi ya kukabili ufisadi. Hii si ni uchawi! Akasema @Carlodera.

Mchango wa vyombo vya habari

Mhasibu Mkuu, Edward Ouko anasema vyombo vya habari vimeripoti visa vingi vya ufisadi vinavyowahusu maofisa wengi serikalini wanaoshirikiana na kufanya njama za kupora mali ya umma tangu Jubilee ichukue hatamu za uongozi 2013.

Baadhi ya washukiwa wa wizi huu waliotajwa wameshtakiwa lakini hawajahukumiwa.

Akizungumza na Shirika la habari la Reuters, Ouko anasema tusipojihadhari, tutaangamizwa na ufisadi. “Viwango vya ufisadi vinasikitisha mno,” anasema.

Uchunguzi ambayo ofisi yake ilifanya unaonyesha kwamba maofisa wa serikali hushirikiana na watu wengine kupora mabilioni ya pesa za umma kila mwaka.

Ouko aliteuliwa 2011 kuwa mhasibu mkuu wa Kenya. Anasema kuna haja ya kubadilisha kabisa mtindo na mfumo wa utoaji na ulipaji zabuni ili kukomesha janga la uporaji.

Jukumu la ofisi yake ni kuhimiza uwazi katika matumizi ya pesa za umma katika viwango vyote vya serikali.

Anasema anapata tatizo kwa sababu mapendekezo aliyotoa kama suluhu ya kumaliza visa hivi 2014 yalipuuzwa na Bunge la Kitaifa na hayajatekelezwa hadi sasa.

“Nina hasira kwa sababu niliweka wazi matatizo yanayochochea ubadhirifu wa pesa lakini hakuna aliyenisikiliza,” akasema Ouko.

Mambo yaigusa familia ya Rais

Katibu wa Wizara ya Mipango na Huduma kwa Vijana, Lilian Mbogo ambaye tayari ameshikiliwa kwa tuhuma hizo amepasua mbarika badala ya kuteseka peke gerezani.

Mbogo anadai kwenye taarifa yake kwa maofisa wa jinai kwamba mjomba wake Rais Uhuru, Paul Gathecha ndiye aliyemlazimisha amlipe kwa zabuni ya petroli.

Gathecha ni mkurugenzi wa kampuni ya Petro Kenya Oil Company Ltd ambayo ililipwa Ksh68 milioni baada ya kuinunulia mafuta Taasisi ya Vijana NYS kwenye zabuni iliyokuwa imetolewa kwa kampuni ya mfanyabiashara, Ben Gethi Horizons Limited.

Hii si mara ya kwanza kwa jamaa wa Rais kuhusishwa katika sakata la ufisadi. Miaka miwili iliyopita dadake na mpwa wake, Rais Uhuru walitajwa kwenye sakata ya Shilingi za Kenya 5.2 bilioni katika Wizara ya Afya.

Dadake Rais, Nyokabi Kenyatta na mpwa wake Kathleen Kihanya ambao ni wakurugenzi wa Sundales International Limited walijitetea kuwa walilipwa Sh41 milioni za Kenya baada ya kupata zabuni ya kununua bidhaa za wizara hiyo.

Je, Rais Uhuru atakuwa na ujasiri wa kuwanasa jamaa wake wa karibu katika vita hivi? Wakenya wanasubiri kwa hamu na ghamu.

Uhuru ataka uchunguzi mali

za vigogo uanze kwake, Ruto

Dorothy Jebet

“Mali zangu zitapelelezwa kisha za Makamu wa Rais na hatimaye mawaziri, magavana, mawaziri na wengine,” anasema Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta baada ya kuzika tofauti zake na Gavana wa Jimbo la Mombasa Hassan Joho.

Matamshi ya Uhuru yamewapa matumaini Wakenya wengi kwamba vita dhidi ya ufisadi sasa vinaweza kuzaa matunda.

Lakini mbali na hayo, baadhi ya Wakenya wana wasiwasi, wanadai kwamba vita hivyo haviwezi kwenda popote kwa sababu viongozi wote wa kisiasa ni wezi tangia zamani.

Hata hivyo, tangazo hilo limewatia kiwewe baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa umma ambao utajiri wao hauelezeki kwa sababu unatokana na wizi wa mali za umma.

Mitandao ya kijamii nchini Kenya imesheheni mazungumzo na mijadala kuhusu tangazo hilo la Rais alilolitoa akiwa ziarani Mombasa.

Kupitia mitandao hiyo, wananchi ‘wanamsaidia’ Rais na maofisa wa jinai kujua mali ya viongozi mbalimbali.

Katika mijadala hii haswa katika Twitter, Wakenya wanaorodhesha baadhi ya viongozi ambao wamekuwa mabwanyenye kwa muda mfupi baada ya kuanza kuwa watumishi wa umma.

Baadhi yao wametajwa kwa kuhamia mitaa ya kifahari ghafla ilhali wamekuwa wakiishi uswahilini kwa muda mrefu.

Mathalan, wanamtaja mwanasiasa mmoja wa ngazi za juu katika serikali ambaye ameupa mkono wa buriani ufukara uliokuwa umemwandama kwa miaka mingi hadi alipoanza kutumikia umma katika nyadhifa mbalimbali.

Mwanasiasa huyo ana helkopta saba za kisasa anazokoidisha serikali na kampuni za serikali kila siku.

Serikali humlipa Ksh230, 000 (Sh5,060,000) kwa saa moja kukodisha ndege hizo. Bila shaka huku Wakenya wakinyeshewa na mvua, mwanasiasa huyo hunyeshewa pesa.

Katibu mkuu mmoja serikalini yasemekana alinunua malori matano mapya kutoka katika kampuni moja inayouza magari kutoka ng’ambo. Pia, Katibu huyo alinunua ekari 38 za ardhi kwa Ksh3 milioni (Sh66 milioni) kwa ekari moja. Je, alipata wapi pesa hizi zote. Isitoshe, alinunua nyumba zipatazo tatu za kifahari ilhali mshahara wake hauwezi kumruhusu kuwa na mamilioni ya pesa.

Vita inamlenga Ruto?

Ingawa juhudi za kupambana na visa vya ufisadi ambavyo wengine huita mlungula, chai au kitu kidogo, kuna viongozi wanaokejeli msimamo wa Rais Uhuru.

Tangu Rais atangaze vita dhidi ya janga hili la ufisadi, chama cha Jubilee kimepasuka mara mbili; kuna upande wa Uhuru na mwingine wa Ruto. Ni upande wa Ruto unaolia mno juu ya mipango ya kupunguza ama kuzika kabisa ufisadi.

Wanadai juhudi za Rais zinamlenga Ruto na marafiki wake wa kisiasa ili kudidimiza ndoto yake ya kutaka kuwa rais 2022.

Mrengo wa Ruto unataka tathimini ya mali ya viongozi na watumishi wengine ipanuliwe ili viongozi wa kuanzia 1963 pia wachunguzwe ili ibainike walipataje utajiri wao.

Mbunge mmoja ambaye ni jirani na rafiki wa Ruto anapendekeza kwamba tathimini ya mali na maisha ya viongozi na watumishi ianzie mwanzilishi wa taifa la Kenya, Mzee Jomo Kenyatta ambaye pia ni babake Rais Uhuru.

Kauli kama hizo bila shaka zinakejeli na kufanyia mzaha juhudi za kupambana na adui huyu wa maendeleo. Pia, ni kama kambi ya Ruto haielewi kwamba mambo yamebadilika na hivi karibuni baadhi yao watajuta kupora mali ya walipa kodi.

Wanasiasa na baadhi ya mafisadi hawajawahi kuchukulia vita hivi kwa umakini; wanadhani kuwa ni mchezo; hawajui wakati huu kumekucha na wanaolengwa afadhali wajitayarishe kukutana na mkono mrefu wa sheria.

Sababu za kujilundikia pesa

Wanasiasa hutumia mamilioni ya pesa katika kampeni za kusaka kura na wanapochaguliwa huwa wanatafuta njia zozote za kurudisha pesa walizotumia wakati wa kampeni.

Vilevile, wanazingirwa na tamaa ya kujilimbikizia mali ili waweze kufanya kampeni ya uchaguzi mkuu unaofuata bila matatizo ya kifedha.

Aidha, pia huwahonga wapinzani wao na wafuasi ili wasiwe na wakati mgumu. Hizi ni baadhi ya sababu ambazo inapalilia ufisadi .

Lakini inagawa baadhi ya viongozi wa Kenya hawaamini kwamba ni wakati wa kupigana na ufisadi, kuna wengine wanaoamini.

Somo hadi nje ya nchi

Wiki jana, Wakenya waliingia kwenye mitandao ya kijamii kuwakejeli na kuwasuta wabunge wanane kutoka Zambia waliozuru nchini kwa minajili ya kuona jinsi Kenya inavyopigana na ufisadi.

Wengi walisema wabunge hao wanafanya mzaha na wamekuja kujifunza njia na mbinu mpya za kupora walipaji kodi wa nchi yao.

Walipowasili, wabunge hao walikwenda moja kwa moja hadi kwa makao makuu ya Tume ya Kupambana na Ufisadi nchini (EACC) na kufanya kikao cha muda na makamishna wa tume hiyo.

Wakenya walicheka mabavu zikawauma baada ya kupokea habari hizo. Wananchi wanasisitiza kwamba, Kenya si kielelezo kizuri cha nchi inayopigana na ufisadi.

“Kile tunachoweza kuwafunza Wazambia ni jinsi ya kuiba na kufanikiwa kama mafisadi Wakenya. Wapenzi Wazambia, hukuna tofauti kati yenu na sisi,” akasema mtumiaji wa Twitter anayejulikana kama @Jma.

“Nasikia wabunge wa Zambia wako hapa kujifunza mikakati ya kumenyana na visa vya ufisadi! Tafadhali, mtazame mawingu, huenda ikanyesha leo,” akasema Jenaro Wachira kwenye Twitter.

@Vikiyo aliandika, “Wabunge hao hawana budi kunaswa na kuwekwa ndani kwa sababu ya kutumia vibaya mali ya umma. Hapa Kenya tunafunza tu jinsi ya kuharakisha ufisadi. Sisi ndio wenyewe.”

“Nini mbaya na Serikali ya Zambia! Siamini iliwatuma wabunge wake hapa kujifunza jinsi ya kukabili ufisadi. Hii si ni uchawi! Akasema @Carlodera.

Mchango wa vyombo vya habari

Mhasibu Mkuu, Edward Ouko anasema vyombo vya habari vimeripoti visa vingi vya ufisadi vinavyowahusu maofisa wengi serikalini wanaoshirikiana na kufanya njama za kupora mali ya umma tangu Jubilee ichukue hatamu za uongozi 2013.

Baadhi ya washukiwa wa wizi huu waliotajwa wameshtakiwa lakini hawajahukumiwa.

Akizungumza na Shirika la habari la Reuters, Ouko anasema tusipojihadhari, tutaangamizwa na ufisadi.

“Viwango vya ufisadi vinasikitisha mno,” akasema.

Uchunguzi ambayo ofisi yake ilifanya unaonyesha kwamba maafisa wa serikali hushirikiana na watu wengine kupora mabilioni ya pesa za umma kila mwaka.