Makamba aagiza maofisa wa kilimo kupelekwa Kabage

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba. 

Muktasari:

  • Agizo hilo  limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba  akiwa katika mkutano wa hadhara na wanakijiji hao.

Katavi. Uongozi wa Mkoa wa Katavi  umeagizwa kuwapeleka maofisa na wataalamu wa kilimo katika Kijiji cha Kabage kwa ajili ya kutoa elimu ya matumizi bora ya maji katika vyanzo vya mto Katuma.

Agizo hilo  limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba  akiwa katika mkutano wa hadhara na wanakijiji hao.

Amesema ametoa agizo hilo baada ya kuona matumizi maji yasiyo sahihi kwa wakazi hao hali inayosababisha mto huo kukauka.