Makamba akipa mifuko 50 ya saruji kikundi cha kilimo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba

Muktasari:

Makamba ametoa uamuzi huo baada ya mwalimu wa kikundi hicho,  Lameck kumweleza changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kutoa mafunzo hayo bila gharama yoyote.

Njombe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba ameahidi kukipa mifuko 50 ya saruji kikundi cha Jerusalemu kinachotoa mafunzo ya kulima nchi kavu badala ya mabonde ili kuhifadhi mazingira na nyanzo vya maji.

Makamba ametoa uamuzi huo baada ya mwalimu wa kikundi hicho,  Lameck kumweleza changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kutoa mafunzo hayo bila gharama yoyote.

"Mmefanya kuwa na kikundi  na nitaleta watu kutoka  maeneo mbalimbali  kuja mbinu hizo ili kulinda vyanzo vya maji," anasema Makamba

Makamba amesema kikundi hicho kikimaliza kuchimba msingi kumpa taarifa ili aweze kupeleka mifuko ya saruji na kwamba atakuwa akikitembelea mara kwa mara ili kujua maendeleo yake.