Makamba aonya shughuli karibu na Ziwa Rukwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba

Muktasari:

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ametoa onyo hilo jana akiwa ziarani eneo la Nankanga Forodhani lililopo kando ya  ziwa hilo wilayani Sumbawanga.

Rukwa. Kuanzia Oktoba 28 mwaka huu ni marufuku kufanyika shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka eneo la Ziwa Rukwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ametoa onyo hilo jana akiwa ziarani eneo la Nankanga Forodhani lililopo kando ya  ziwa hilo wilayani Sumbawanga.

Pia, amepiga marufuku mifugo kupelekwa ziwani ndani ya mita 200.

Makamba amesema uamuzi huo unalenga kurudisha uhai wa ziwa hilo lililopo hatarini kutoweka kutokana na shughuli za kibinadamu.