Makamba kuupa kipaumbele cha mazingira mkoa wa Katavi

Muktasari:

Makamba amesma hayo leo baada ya kupokea taarifa ya ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kutoka kwa mkoa wa mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga.

Katavi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema ataupa kipaumbele Mkoa wa Katavi katika miradi ya mazingira ili uweze kutunza mazingira kwa ufanisi.

Makamba amesma hayo leo baada ya kupokea taarifa ya ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kutoka kwa mkoa wa mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga.

Amesema ameridhishwa na taarifa hiyo iliyokuwa na maswali na majibu kuhusu utekelezaji na uhifadhi wa mazingira hivyo hanabudi kuwapa kipaumbele cha miradi ya maendeleo kama alivyoombwa katika taarifa.

Meja Jenerali Muhuga amesema miongoni mwa kipaumbele ni nyezo za uhifadhi wa mto Katuma ili uweze kutitirisha maji kwa ufanisi sanjari na kuweka alama kwa ajili ya kuzuia watu wasivamie vyanzo vya maji.