Makene aendelea kusota rumande

Muktasari:

  • Mkuu wa kitengo chaa habari wa Chadema, Tumaini Makene anaendelea kushikiliwa na Jeshi la polisi kitengo cha makosa ya mtandao akihojiwa kuhusu umiliki wa blog ya Chadema.blogspot.com

Dar es salaam. Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kitengo cha makosa ya mtandao.

Akizungumza na MCL Digital wakili wa Makene, Fred Khiwelo amesema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia kwa ajili ya uchunguzi kuhusiana blog iitwayo Chadema.blogspot.com pamoja na maudhui yake.

“Ni kweli nimemfuatilia mteja wangu kujua haki ya kupata dhamana baada ya kushikiliwa toka jana lakini polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi na hivyo hawawezi kutoa dhamana kwa muda huu,” amesema Khiwelo.

Amesema swala la kumiliki mtandao mwanachama yeyote anaweza kuwa anamiliki kwa jina hilo, kumshikilia mteja wake kwa muda wote bila kumpa dhamana ni ukiukwaji wa sheria.

Mchana wa leo, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema akizungumza makao makuu ya Chadema amesema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia Makene.