Makonda aongeza muda upimaji afya bure

Muktasari:

Awali, kampeni hiyo ilitarajiwa kuhitimishwa Septemba 25, kwa kuwafikia watu 3,000 lakini mwitikio wa wananchi ni mkubwa ambao wamefikia zaidi ya 9,000.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameongeza siku mbili zaidi na wahudumu ili kutoa huduma ya upimaji afya bure.

Awali, kampeni hiyo ilitarajiwa kuhitimishwa Septemba 25, kwa kuwafikia watu 3,000 lakini mwitikio wa wananchi ni mkubwa ambao wamefikia zaidi ya 9,000.

Amesema ameomba Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuongeza madaktari 30 na wauguzi 60. Watoa huduma wengine wanatoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Saratani Ocean Road, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, hospitali za rufaa Mkoa wa Dar es Salaam, Hospitali ya Aga Khan na Taasisi za CCP Medicine.