Makongoro; miaka miwili ajali mbili

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere .

Muktasari:

Makongoro, mwana wa Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa anakwenda jijini Arusha akitokea Dodoma kwenye mkutano maalumu wa CCM Taifa uliomchagua Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Babati. Ikiwa ni mwaka mmoja umepita msafara wake upate ajali Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wakati akitafuta wadhamini ndani ya CCM katika kuwania kupata ridhaa ya chama hicho kugombea urais, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere amenusurika kifo baada ya gari lake kuwagonga ng’ombe saba na kondoo mmoja  waliokufa papo  hapo eneo la Makatanini wilayani Babati, Mkoa wa Manyara.

 Makongoro, mwana wa Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa anakwenda jijini Arusha akitokea Dodoma kwenye mkutano maalumu wa CCM Taifa uliomchagua Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis Massawe alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa moja usiku barabara kuu ya Arusha-Babati.