Mali za Mbowe zaendelea kusombwa

Muktasari:

Mwananchi iliyopo eneo la tukio sasa hivi imeshuhudia magari yakiendelea kusomba baadhi ya mali huku maofisa wa NHC ambao hawakutaka kutaja majina yao wakisema wanachukua mali zinazoweza kupigwa mnada tu.

Dar es Salaam. Maofisa wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) bado wanaendelea kuondoa vitu katika ofisi za jengo hilo linalomilikiwa na NHC kutokana na deni la Sh1 bilioni analodaiwa.

Mwananchi iliyopo eneo la tukio sasa hivi imeshuhudia magari yakiendelea kusomba baadhi ya mali huku maofisa wa NHC ambao hawakutaka kutaja majina yao wakisema wanachukua mali zinazoweza kupigwa mnada tu.

Wengine waliokuwa wakifanya zoezi hilo la kuondoa mali za Mbowe ni madalali wa kampuni ya Foster ambao nao walikataa kuzungumza lolote wakidai kuwa viongozi wao ndiyo wenye mamlaka ya kutoa taarifa.

Mwananchi ilishuhudia nyaraka na vyombo, kama chupa, taa za klabu ya Bilicanas vikiwa vimesambaa nje ya jengo hilo.