Mambo 10 muhimu ya kufahamu kuelekea Kombe la Dunia

Muktasari:

Fainali za Kombe la Dunia zinatarajiwa kuanza Juni 14 

Fainali za Kombe la Dunia zinatarajiwa kuanza Juni 14 ambapo mchezo wa ufunguzi utawakutanisha Urusi na Saudi Arabia. Hata hivyo tunapoelekea kwenye fainali hizo kuna mambo muhimu ambayo unapaswa kuyafahamu.

1. Fainali hizo zinafanyika hii ikiwa ni mara ya 21 tangu zilipoanza kufanyika.

2. Jambo jingine muhimu ni kwamba baada ya fainali hizi na zinazokuja za 2022 itakuwa mwisho wa timu 32 kushiriki, kuanzia mwaka 2026 na kuendelea jumla ya timu 48 zitashiriki.

3. Ice Land na Panama ndio mara yao ya kwanza kushiriki fainali za Kombe la Dunia tangu kuanzishwa kwake.

4. Brazil ndiyo nchi pekee ambayo imeshiriki fainali zote za Kombe la Dunia na kunyakua mataji mara 5.

5. Ujerumani ndiyo nchi pekee iliyofunga mabao mengi katika mashindano kwa misimu mitatu iliyopita ambapo mabao 18 mwaka 2014, mbao 16 mwaka  2010 na mabao 14 ikiwa nyumbani mwaka 2006.

6. Inakadiriwa kwamba takribani watu bilioni 3 walitazama fainali za Kombe la Dunia zililopita ambapo ni nusu ya idadi ya watu duniani kote

7. Urusi hii haijawahi kuvuka hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia. Kinachosubiriwa ni iwapo itatumia vyema nafasi ya kuwa mwenyeji wa mashindano?

8. Iran inafuzu kwa mara ya kwanza fainali za Kombe la Dunia mfululizo katika historia yake ya soka, ilifuzu 2014 na sasa 2018.

9. Nchi ndogo zaidi kushiriki Kombe la Dunia ni Iceland ambayo ina idadi ya watu 334,000.

10 Uholanzi ni taifa ambalo limeshiriki fainali nyingi za Kombe la Dunia bila kuambulia taji, lakini safari hii imeshindwa japo kufuzu kushiriki fainali za 2018.