Mambo matano unayopaswa kuyafahamu leo

Iyena yaupiku Mvumo wa Radi

Diamond Platnumz akishirikiana na Rayvanny katika wimbo Mvumo wa Radi, wameupiku wimbo huo katika orodha ya nyimbo zilizotazamwa zaidi tangu ziwekwe katika mtandao wa Youtube mwezi uliopita.

Mpaka kufikia juzi wimbo Iyena uliowekwa mtandaoni Mei 31 ulikuwa umetazamwa mara milioni 3.04 wakati Mvumo wa Radi uliowekwa Mei 11, milioni 2.6.

Mayeather ndiye mwenye fedha zaidi

Jarida maarufu duniani la Forbes limetangaza majina ya wanamichezo 100 walioingiza mkwanja mrefu duniani kwa mwaka 2017/2018 ambapo mwanamasumbwi Floyd Mayweather ameongoza kwenye orodha hiyo. Mayweather ameongoza kwa kuingiza kiasi cha dola milioni 285 sawa na Sh650 bilioni akifuatiwa na mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi aliyeingiza dola milioni 111 sawa na Sh253 bilioni.

Maria Consolata wafariki dunia

Pacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti walifariki dunia katika hospitali ya mkoa wa Iringa walipokuwa wakipatiwa matibabu. Maria na Consolata waliokuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Katoliki Iringa, walikuwa wakisumbuliwa na matatizo ya moyo.

Sam wa Ukweli afariki dunia

Imekuwa wiki mbaya kwa tasnia ya Bongo Fleva nchini baada ya mwanamuziki Sam Ukweli kufariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi. Inaelezwa kuwa mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na nyimbo Sina Raha na Hata Kwetu Wapo alifariki dunia wakati akiwa njiani kuelekea hospitalini.

Trump, Kim kukutana Sentosa

Eneo la mkutano kati ya Rais Trump na Kim Jong Un will litakuwa Hoteli Capella iliyopo kisiwa cha Sentosa nchini Singapore. Viongozi hao waliojijengea uhasama watakutana Juni 12 mwaka huu. Unatarajiwa kuwa mkutano wa Kihistoria kwa viongozi hao wa mataifa ya Marekani na Korea Kaskazini.