Man City, Arsenal zafanya mauaji

Kevin De Bruyne

Muktasari:

Ilkay Gundogan aliingia katika orodha ya wafungaji na kuharibu mwanzo mpya wa maisha ya kiungo wa zamani wa Arsenal, Jack Wilshere aliyesajiliwa

Manchester City imeendeleza ubabe wake kwa kuifumua Bournemouth mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika kwenye Uwanja wa Etihad jana na kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Kevin de Bruyne alianza kufunga kwa mkwaju wa adhabu kabla ya Kelechi Iheanacho na Raheem Sterling kufunga mabao mengine mawili.

Ilkay Gundogan aliingia katika orodha ya wafungaji na kuharibu mwanzo mpya wa maisha ya kiungo wa zamani wa Arsenal, Jack Wilshere aliyesajiliwa Bournemouth.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Man City, Arsenal nao walikuwa na siku nzuri kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Hull City.