Manyanya atangaza kiama vyuo vikuu

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya

Muktasari:

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya  amesema Serikali imetoa Sh40 bilioni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kusisitiza kuwa, vyuo vilivyokuwa na wanafunzi hewa vitakatwa fedha.

Dodoma. Vyuo vikuu vitakavyobainika kuwa na wanafunzi hewa vitatakiwa kulipa madeni ya waliopewa mikopo.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya  amesema Serikali imetoa Sh40 bilioni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kusisitiza kuwa, vyuo vilivyokuwa na wanafunzi hewa vitakatwa fedha.

Naibu Waziri amesema hakuna mtu anayeweza kukwepa katika hilo, kwani Serikali inajua kiwango walichotumia bila ya kuwa na wanafunzi na kwamba, ilikuwa inawasubiri kwa sababu ilitaka kupata sehemu ya kuwakamatia.

Ametaja chanzo cha tatizo la kudorora kwa elimu ya juu nchini kuwa ni kutowekeza kikamilifu kwenye elimu ya vyuo vya kati.