Maofisa watatu wa TIB wafikishwa mahakamani

Muktasari:

Akisoma hati ya mashtaka leo kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Odessa Horonge  alidai kuwa Oktoba 2016  katika ofisi za Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB)  tawi la Upanga, zilizoko  wilayani Ilala, washtakiwa hao wakiwa waajiriwa, Edward na Aloyce kama maofisa wa ufilisi na Salum  waliomba hongo ya Sh 5 milioni kutoka kwa Gosbert Matale.

Dar es Salaam. Maofisa watatu  wa Tanzania Investment Bank (TIB),  Edward Sizya, Aloyce Lufungulo na Salum Abdul wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashtaka manne ya kuomba na kupokea hongo ili kumsaidia mteja kupata hati ya nyumba iliyokuwa inashikiliwa na benki hiyo kama dhamana ya mkopo.
Akisoma hati ya mashtaka leo kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Odessa Horonge  alidai kuwa Oktoba 2016  katika ofisi za Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB)  tawi la Upanga, zilizoko  wilayani Ilala, washtakiwa hao wakiwa waajiriwa, Edward na Aloyce kama maofisa wa ufilisi na Salum  waliomba hongo ya Sh 5 milioni kutoka kwa Gosbert Matale.
Horonge alidai kuwa washtakiwa hao waliomba hongo ya kiasi hicho cha fedha  kama kishawishi cha kumsaidia Evelina Ndecha kukomboa hati yake ya nyumba inayoshikiliwa na benki hiyo kama dhamana ya mkopo.