Marekebisho sheria ya vyama vya siasa kujulikana mwezi ujao

Muktasari:

Sasa kamati hizo zinatakiwa kujadili marekebisho ya kanuni za usajili wa vyama vya siasa baada ya baraza hilo kushindwa kujadili.

Dar es Salaam.  Baraza la Vyama vya Siasa limesitisha mjadala wa  mapendekezo ya marekebisho ya sheria mpya ya vyama vya siasa na kurudisha mchakato huo katika kamati ya sheria na utawala bora, kamati  ya uongozi ya baraza hilo.

Sasa kamati hizo zinatakiwa kujadili marekebisho ya kanuni za usajili wa vyama vya siasa baada ya baraza hilo kushindwa kujadili.

Akizungumza leo Januari 18, 2018 mwenyekiti wa baraza hilo, John Shibuda amesema mapendekezo hayo yanatakiwa kukamilika baada ya mwezi mmoja kabla ya kuitisha baraza maalum litakalopitia suala lililopaswa kufanywa leo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 38, akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, Makamu Mwenyekiti wa CCM  Bara, Philip Mangula na  Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Dk Abdallah Juma  Saadala.