Sunday, August 13, 2017

Marais EAC wamtumia salam Uhuru

 

By George Njogopa, Mwananchi gnjogopa@mwananchi.co.tz

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wametumia akaunti zao za Twitter kupongeza ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakisema ni ishara njema kwamba jumuiya hiyo itaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kuimarika.

Ikiwa ni utamaduni mpya unaoanza kujengeka kwa viongozi hao wa Afrika Mashariki, kwa nyakati tofauti waliandika kwenye akaunti zao wakimpongeza Rais Kenyatta na kumtakia mafanikio mema wakati anapoingia kwenye ngwe yake ya mwisho ya uongozi.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambaye ni mwenyekiti wa EAC alisema ana matumaini ya kuendelea kushirikiana na Rais Kenyatta kuboresha ustawi wa wananchi wa pande zote mbili na kukamilisha kiu ya maendeleo kwa jumuiya nzima.

Alieleza kuwa kuchaguliwa kwake kunaonyesha jinsi wananchi wa Kenya walivyokuwa na imani na uongozi wake hivyo ataendelea na jitihada za kuimarisha amani na umoja kwa wananchi wa EAC.

“Kwa niaba ya wananchi wa Uganda na watu wa Afrika Mashariki napenda kukupongeza kwa kuchaguliwa tena na imani yangu katika kipindi cha miaka yako mitano ya uongozi utahakikisha unaendelea kusaidia eneo hili linaimarika na kuwaletea maendeleo watu wake,” aliandika Rais Museveni. Ujumbe wa pongezi pia uliandikwa na Rais John Magufuli ambaye alimalizia kwa kumtakia Rais Kenyatta mafanikio mema. “Nakupongeza Ndugu Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema,” ulisomeka ujumbe wa Rais Magufuli kwa Rais Kenyatta.

Akiandika kwa Lugha ya Kiswahili, Rais wa Rwanda, Paul Kagame alitaka viongozi hao kuendelea kuchapa kazi pamoja ili kuzidi kuijenga Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“@UKenyatta pamoja tuzidi kujenga umoja na maendeleo ya mataifa na jumuiya yetu,” aliandika Rais Kagame ambaye naye wiki iliyopita alichaguliwa tena kuendelea kubaki madarakani.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza mbali ya kumpongeza pia aliandika kuelezea matumaini yake kuhusu kuendelea kuimarika kwa uhusiano wa pande hizo mbili.

“Kwa niaba ya wananchi wa Burundi, nakupongeza Rais Mteule Kenyatta na wananchi wa Kenya kwa ujumla na tunatarajia kuendelea kudumisha uhusiano wetu,” alisema Rais Nkurunziza.

Hakukuwa na ujumbe wowote kutoka kwa Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir ambaye taifa lake lilijiunga na EAC mwaka jana.

Mtindo wa kutuma ujumbe kwa kutumia akaunti binafsi za viongozi ulianza kupata nguvu zaidi katika miezi ya hivi karibuni hasa baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa mtumiaji mkubwa kwa mtandao wa Twitter akielezea mambo yanayohusu Serikali na mengine binafsi.

viverra ullamcorper est sit amet vulputate! Curabitur ut orci turpis, vitae blandit quam. Ut ullamcorper, metus vitae elementum tincidunt, augue nisl scelerisque nisl, sit amet laoreet mauris odio ac mauris. Quisque pellentesque iaculis dolor, non vulputate tortor ultricies nec. Maecenas tincidunt pellentesque erat, vel sagittis ipsum elementum id. Fusce congue nisl a enim sodales feugiat non nec sapien.

Cras dictum lorem vel urna convallis eget suscipit urna hendrerit. Nulla sit amet odio nec ipsum sollicitudin vestibulum. Nunc porta, augue quis interdum gravida, ipsum tellus posuere libero; sit amet ultricies ligula sapien sodales nisl. Morbi sodales, quam sed accumsan scelerisque, enim erat placerat orci, a interdum leo orci ac tellus? Nullam feugiat elementum purus, vitae condimentum mi sodales fermentum? Praesent gravida commodo purus, vel lacinia leo facilisis nec. Quisque hendrerit, nibh ac suscipit vestibulum, lacus risus ultricies urna, a lobortis dolor massa eu magna. Donec viverra, nulla nec varius scelerisque, est sem fringilla magna, quis imperdiet urna sapien sit amet orci. Aliquam mollis feugiat dui sit amet vulputate. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus ornare, sem a rhoncus rhoncus, erat tellus posuere arcu, id tincidunt mauris urna eu lacus! Nunc hendrerit condimentum purus, vel pharetra leo ultricies eu! Donec vitae turpis sapien.

Proin varius, nunc vitae pellentesque feugiat, nulla justo ullamcorper felis, et iaculis lacus justo at nisi? Curabitur eu turpis at nulla faucibus tristique? Phasellus faucibus consectetur dui. Aliquam sed magna

-->