Marekani yaanza kujenga mtambo kuzuia makombora ya Korea Kusini

Muktasari:

Mtambo huo wa hali ya juu ambao kwa kitaalamu huitwa ‘Terminal High Altitude Area Defense’ unajengwa ili kujihami kutokana na wasiwasi uliopo wa tishio kutoka Korea Kaskazini ambao wanafanya majaribio ya makombora.

Korea. Jeshi la Marekani limeanza kujenga mtambo mkubwa wa kujilinda dhidi ya makombora  yanayoweza kurushwa na Korea Kaskazini.

Mtambo huo wa hali ya juu ambao kwa kitaalamu huitwa ‘Terminal High Altitude Area Defense’ unajengwa ili kujihami kutokana na wasiwasi uliopo wa tishio kutoka Korea Kaskazini ambao wanafanya majaribio ya makombora.

Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.