Markzuckerberg ala ugali na samaki

Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg

Muktasari:

Katika kikao hicho, Zuckerberg na Waziri Mucheru alizungumza kuhusu mtandao na mpango wa serikali kuhakikisha kila kijiji kimeunganishwa na mtandao.

Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg jana alikula ugali na samaki aliposhiriki chakula cha mchana na Waziri wa Habari wa Kenya, Joseph Mucheru.

Katika kikao hicho, Zuckerberg na Waziri Mucheru alizungumza kuhusu mtandao na mpango wa serikali kuhakikisha kila kijiji kimeunganishwa na mtandao.

Zuckerberg alikula kwa mara ya kwanza ugali na samaki katika hoteli ya Mama Oliech iliyopo katika jiji hilo.

''Swala muhimu ninapozuru taifa lolote jipya ni kujaribu kula chakula chao.Nilipenda sana ugali na samaki mzima wa tilapia'',alisema Zuckerberg.