Zaidi ya watu 400 wauawa Syria

Muktasari:

Shirika la Kufuatilia Haki za Binadamu la Syria lilisema Alhamisi kwamba kwa uchache watu 403 waliuawa katika "shambulio la kupagawisha" lililoanza Jumapili, wakiwemo watoto 150. Takriban watu wengine 2,220 walijeruhiwa.


Mjumbe maalum Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya amani Syria, Staffan de Mistura, alisisitiza haja ya dharura ya kusitisha mapigano alipotoa maoni yake kabla ya mkutano wa Baraza la Usalama Alhamisi.

 

Watu zaidi ya 400 wameuawa Ghouta Mashariki, kundi la ufuatiliaji wa haki za binadamu lilisema, wakati vikosi vya serikali vya Syria vikisaidiwa na ndege za kivita za Urusi zikishambulia kutoka angani eneo linaloshikiliwa na waasi.

Shirika la Kufuatilia Haki za Binadamu la Syria lilisema Alhamisi kwamba kwa uchache watu 403 waliuawa katika "shambulio la kupagawisha" lililoanza Jumapili, wakiwemo watoto 150. Takriban watu wengine 2,220 walijeruhiwa.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya amani Syria, Staffan de Mistura, alisisitiza haja ya dharura ya kusitisha mapigano alipotoa maoni yake kabla ya mkutano wa Baraza la Usalama Alhamisi.

"Hali ya kibinadamu Ghouta Mashariki inatisha, na kwa hiyo, tunahitaji kusitisha mapigano ambayo yatakomesha mashambulizi ya kutisha Ghouta Mashariki na makombora Damascus," alisema.

Aliongeza kuwa kusitishwa kwa mapigano hayo kunapaswa kufuatiwa na upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na kusaidia kuondolewa kwa majeruhi kutoka Ghouta Mashariki, na alionya hali hii kurudia Aleppo.

Wakazi wa Ghouta ya Mashariki, ambao wengi wao ni waliotawanyika ndani, wanasema hakuna kitu wanachoweza kufanya na hakuna mahali pa kujificha.

Rafat al-Abram anaishi Douma na ni fundi magari. Mashambulizi ya angani kwa siku chache zilizopita yamevuruga kazi yake kwa kuwa mtaa ambako anafanyia shughuli zake ulipigwa katika mashambulio hayo.

"Nilibahatika kutoa nje baadhi ya zana na vifaa vyangu, na kuendelea kurekebisha magari kokote ninakoweza," aliiambia Al Jazeera.