Mashine 15 kutibu dalili za saratani zatolewa

Dar es Salaam. Shirika la Kimataifa la Tafiti za Saratani (IARC) leo limeikabidhi mashine 15 za kutibu dalili za awali za satarani ya shingo ya kizazi.

Mashine hizo zitasambazwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ikiwa ni katika kutekeleza mkakati wa kupunguza vifo vitokanavyo na saratani.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Wizara hiyo imepanga kuwafikia wanawake 2milioni baada ya miaka miwili.

Mwalimu alisema kati ya wagonjwa 100 wanaofika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road 33 wana saratani ya shingo ya kizazi.

"Tunataraji kwamba tusambaze mashine hizi kwa mikoa 10 isiyo na huduma ya matibabu ya saratani, lakini pia tunatarajia ndani ya miaka miwili angalau vituo vya afya 90 vitoe matibabu haya," alisema Mwalimu.

Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo, Mkurugenzi wa Cervical Cancer Action, Celine Schocken alisema mradi huo unazunguka kwa takribani nchi 30 Duniani kwa msaada wa watu wa Marekani.

"Tulianza mwaka 2013 tukiwa na Mama Salama Kikwete na kwa mwaka huu wa 2015/2016 tutapeleka huduma hii mikoa tisa lengo ni kupunguza vifo vitokanavyo na saratani," alisema Schocken.