Masogange afariki na ‘mshikaji wake’ wa Sweden

Muktasari:

Masogange  alifariki siku ambayo raia wa Sweden, DJ Avicii alikutwa amefariki katika mji wa Muscat, nchini Oman.


Mpambaji wa muziki wa kipya kizazi, Agnes Masogange alifariki Aprili 20, katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam na siku hiyohiyo alifariki rafiki yake wa karibu kabisa katika mtandao wa kijamii wa Instagram, DJ Avicii.

Masogange  alifariki siku ambayo raia wa Sweden, DJ Avicii alikutwa amefariki katika mji wa Muscat, nchini Oman.

Mbali na urafiki waliokuwa nao Agnes na Avicii katika Instagram walizaliwa wiki inayofanana sawa na mwezi na mwaka.

Agnes alizaliwa Septemba 9, mwaka 1989 wakati Tim Berg maarufu kama DJ Avicii naye alizaliwa Septemba 8, 1989, wote wakiwa na umri wa miaka 28, huku wakitofautiana kwa siku moja tu kuzaliwa.

Agnes, ambaye amezikwa leo Jumatatu Aprili 23, 2018 kwao Mbeya, alikuwa akionekana akistarehe katika kumbi mbalimbali za starehe usiku na huenda miongoni mwa nyimbo ambazo alikuwa akifurahishwa nazo ni zile ambazo zilikuwa zinachezwa na DJ Avicii ambaye mpaka anafariki alikuwa akiishi mjini Muscat.

Ukaribu ambao walikuwa nao Masogange na DJ Avicii mbali na kuzaliwa siku zilizofuatana, mwaka na mwezi unaofanana, huenda kifo chao kilikuwa kama walisindikizana baada ya kufa siku moja ingawa walipishana saa chache.

DJ Avicii mbali na ukaribu na Agnes katika mtandao wa Instagram alikuwa kioo cha jamii kwa baadhi ya Ma-DJ kutoka Tanzania kama Romijons ambaye siku ya tukio hilo aliandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa ni miongoni mwa watu waliomfanya kupenda fani hiyo.