Matrekta kuanza kuundwa nchini

Muktasari:

Mkataba huo unakadiliwa kuwa na thamani ya takriban Sh 50 bilioni mpaka 100 na umelenga kuongeza upatatikanaji wa bidhaa hiyo kwa urahisi sanjali na punguzo la bei ili kuwanufaisha wakulima wadogo, wakati na wakubwa.

Dar es Salaam. Kampuni ya Sonalika international Tractor limited ya India imesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Quality Group kwa ajili ya kuunda trekta za kilimo hapa nchini.

Mkataba huo unakadiliwa kuwa na thamani ya takriban Sh 50 bilioni mpaka 100 na umelenga kuongeza upatatikanaji wa bidhaa hiyo kwa urahisi sanjali na punguzo la bei ili kuwanufaisha wakulima wadogo, wakati na wakubwa.

Ofisa Masoko wa Qualiy Group Timoth Shuma amesema “Undaji wa trekta hizo unatarajiwa kuanza mapema mwaka ujao. Trekta 1,000 zitakuwa zinaundwa kila mwaka kuanzia zenye horsepower 20 mpaka 110 huku zikiwa na punguzo la bei la zaidi ya asilimia 30”.