Matumaini mapya kodi ya vifungashio vya dawa
Muktasari:
Anapendekeza kuondolewa kodi ya thamani katika vyakula vya mifugo na dawa za mifugo.
Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango amesema atapeleka muswada wa sheria kupendekeza kuondolewa kwa kodi katika vifungashio vya dawa za binadamu zinazotengenezwa na viwanda nchini .
Akizungumza bungeni leo juni 14 Alhamisi jioni hii, wakati akiwasilisha bajeti kuu kwa mwaka wa fedha 2018/19, Dk Mpango amesema lengo la hatua hiyo ni kuongeza uwekezaji katika sekta ya dawa za binadamu.
Amesema pia anapendekeza kuondolewa kodi ya thamani katika vyakula vya mifugo na dawa za mifugo.
Soma Zaidi: Dk Mpango: Rais alinitwisha msalaba wa zege