Mawakili wamkalia kooni Bulaya

Muktasari:

Katika Uchaguzi Mkuu wa ubunge Jimbo la Bunda Oktoba 25, 2015, Bulaya alimbwaga mgombea wa CCM na mwanasiasa mkongwe, Stephen Wasira lakini wapigakura wanne walifungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga matokeo.

Musoma. Mawakili wa wadai katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi 2015 inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya, wamemtaka mlalamikiwa huyo kutoa ufafanuzi wa idadi ya wapigakura waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Katika Uchaguzi Mkuu wa ubunge Jimbo la Bunda Oktoba 25, 2015, Bulaya alimbwaga mgombea wa CCM na mwanasiasa mkongwe, Stephen Wasira lakini wapigakura wanne walifungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga matokeo.

 Ester alikuwa mbunge wa viti maalumu CCM, lakini alihamia Chadema na kumshinda mkongwe Wasira.