Mawaziri watano wafanya ziara mpakani mwa Tanzania na Uganda

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Muktasari:

Mawaziri hao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleman Jaffo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe.

Mawaziri watano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatembelea mpaka wa Tanzania na Uganda ili kutatua changamoto zinazoukabili mpaka huo na kuuboresha.

Mawaziri hao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleman Jaffo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe.

Miongoni mwa maeneo yanayotembelewa na mawaziri hao ni eneo la mpaka wa Tanzania na Uganda kwa upande unapopita Mto Kagera na eneo la kivuko cha mpaka wa Tanzania na Uganda kilichopo Mtukula, Kagera.

Mawaziri hao wameweza kujionea hali halisi ya maisha ya wakazi wa mipakani na jinsi wanavyohusiana na wenzao wa nchi jirani ya Uganda ambapo wamekuwa wakishirikiana na kuishi kwa amani katika shughuli zao za kila siku.

Aidha, ziara hii ni maandalizi ya mkutano wa ujirani mwema kati ya mawaziri wa Serikali ya Uganda na wenzao wa Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, Bukoba, Kagera.