Mazoezi ya polisi yafunga maduka Dar es Salaam

Askari Polisi wa kikosi maalum cha polisi (CRT)  wakiwa katika mazoezi ya utayari wa kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza.

Muktasari:

Chadema wametangaza Septemba Mosi kuwa ni siku ya maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima

 

Dar es Salaam. Zikiwa zimesalia siku sita kufanyika kwa maandamano ya Ukuta, hofu na taharuki jana viliwakumba wakazi na wafanyabiashara wa eneo la Maturubai, Mbagala Rangi Tatu baada ya kushuhudia vikosi vya polisi  vikifanya mazoezi ya kuzuia  na kupambana na uhalifu.

Akizungumzia mazoezi hayo,   Kamishna  wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema yalianzia Wilaya ya Temeke na Kigamboni na leo yataendelea Ilala na kumalizia Kinondoni.

Habari zaidi soma Gazeti

la Mwananchi