Mbarawa aonya wanaokaa mabondeni
Muktasari:
- Waziri Mbarawa aliwataka watu hao waliogoma kuhama kuzingatia utabiri wa hali ya hewa juu ya hatari inayowanyemelea
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame
Mbarawa amewataka watu wanaoishi mabondeni waliogoma kuondoka baada ya
kupata taarifa juu ya hatari inayowanyemelea kuondoka mara moja ili
kuepusha majanga.
Akizungumza leo Machi 23, Mbarawa amesema hivi sasa Mamlaka ya Hali ya
Hewa Nchini (TMA) inatoa taarifa za hali ya hewa inayowataka walioko
katika maeneo ya mabondeni lakini hawako tayari kuondoka.
“Unapopata taarifa ya hali ya hewa kama mahali hapo si lazima maana
yake ni lazima uondoke, vinginevyo utapata shida,”amesema.
Amesema lazima kufuata utabiri wa hali ya hewa ili kujiepusha na
majanga yanayoweza kujitokeza kwa kudharau taarifa zinazotolewa na
mamlaka hiyo.
Amesema zingatia taarifa hali ya hewa ndio kaulimbiu ya
maadhimisho yaliyofanyika jana yakilenga watu kutopuuza utabiri
wa hali ya hewa.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema makubaliano ya kimataifa ni kuwa na utabiri wenye usahihi kwa asilimia isiyopungua asilimia 70.
“Utabiri wetu sasa umeongezeka usahihi tumefika hadi asilimia 88
wakati mwingine tunafika asilimia 90,”amesema.
Aidha, amesema wamekuwa wakishirikiana na taasisi nyingine nchini
katika kuchukua hatua wanapotoa taarifa za kutahadharisha watu.