Thursday, January 5, 2017

Mbaroni akidaiwa kufukua kaburi

 

By Ipyana Samson, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mbeya. Mkazi wa Kijiji cha Chapakazi, Mbeya Vijijini amekamatwa na polisi kwa kwa tuhuma za kufukua kaburi alilozikwa mtu aliyekuwa na ulemavu wa ngozi, (albino), mwaka 2010.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Dhahiri Kidavashari amesema jana kuwa  mtuhumiwa huyo (jina linahifadhiwa) alikamatwa usiku wa kuamkia jana akiwa na majembe na koleo.

Kidavashari amesema kaburi alilokuwa akifukua alizikwa Sister Osisara ambaye alikuwa albino.

Amesema marehemu alifariki dunia mwaka 2010 kwa ugonjwa wa homa na kuzikwa katika makaburi ya Kijiji cha Mumba ambako mtuhumiwa alikutwa akifukua kaburi lake.

-->