Mbowe: Lissu anaweza kuongea na kula kidogo

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Muktasari:

 

  • Lissu anaendelea na matibabu jijini Nairobi baada ya kujeruhiwa na risasi akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma

Nairobi. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa hivi sasa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaweza kuongea na kula kidogo.

Akizungumza na waandishi leo Alhamisi jijini Nairobi, Mbowe amesema taarifa za kwamba Lissu amepata maambukizi katika kifua ambayo yanatishia maisha yake siyo za ukweli. 

Mbowe amesema hali ya Lissu inabadilika kila siku hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anaendelea kurejea katika hali yake.

Amesema Lissu ameweza kuonana na baadhi ya waliomtembelea kwa maelekezo ya madaktari ambao wanamtibu.

"Pamoja na kwamba kuna watu wengi wanataka kumuona lakini ni wachache wanaoruhusiwa kumuona kwa kuwa madaktari wanataka apumzike,"amesema Mbowe.