VIDEO: Mbowe akisema haendi polisi kwa wito wa Makonda

Mbowe, Siuzi wala situmii madawa ya kulevya

Muktasari:

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mbowe amesema yuko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kama utaratibu wa kisheria utafuatwa.

Dodoma. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hatafika polisi kwa kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mbowe amesema yuko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kama utaratibu wa kisheria utafuatwa.                       

“Makonda hana mamlaka ya kumpa wito mtu kwenda polisi kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa,”amesema Mbowe.

“Makonda amenichafulia jina langu, chama, familia na upinzani.”                       

Mbowe ni mmoja kati ya watu 65 waliotakiwa na Makonda kufika kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.