Mbowe mikononi mwa polisi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Muktasari:

Mbowe alifikishwa kituoni hapo baada ya kupewa saa 48 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro awe amejisalimisha polisi ambazo mwisho wake ulikuwa leo.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekamatwa na polisi akiwa kwenye gari lake barabarani na kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.

Mbowe alifikishwa kituoni hapo baada ya kupewa saa 48 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro awe amejisalimisha polisi ambazo mwisho wake ulikuwa leo.

Kamanda Sirro alitoa muda huo Jumamosi iliyopita akimtaka Mbowe afike kituoni hapo, vinginevyo wangemsaka kwa namna ambayo jeshi hilo lingeona inafaa.

Baada ya Mbowe kupelekwa polisi, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema mwenyekiti huyo alikamatwa barabarani na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi.