Mbunge aibua tena suala la samaki bungeni

Muktasari:

Dau amesema hayo wakati akichangia Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19, bungeni leo Juni 21, 2018 na kumuomba Mpina kwenda Mafia na maofisa wake kutoa elimu juu ya suala hilo.

Dodoma. Mbunge wa Mafia (CCM), Mbaraka Dau amemtaka Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kutambua kwamba kuna samaki ambao kimazingira hawawezi kufikia sentimita 25 inayotakiwa na Serikali.

Dau amesema hayo wakati akichangia Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19, bungeni leo Juni 21, 2018 na kumuomba Mpina kwenda Mafia na maofisa wake kutoa elimu juu ya suala hilo.

“Kuna samaki hawezi kufikia sentimita 25, waziri njooni mje muongee na wavuvi muwaeleze kila samaki wakipelekwa wanakuwa ‘reject’ (wanakataliwa) njooni kwani samaki wengine hawafikii sentimita hizo. Waziri uje Mafia na wataalamu wako,” amesema Dau.

Amesema samaki hawapo katika maziwa tu, wako katika bahari na wengine wana ukubwa ambao haufikii  unaotakiwa na waziri.

Pia amesema sekta ya uvuvi imesahaulika hata katika bajeti kwa kutengewa asilimia 0.01 ya fedha za maendeleo na kueleza kwamba kuna tatizo kubwa katika sekta hiyo.