Mbunge amwaga powertiller kila kijiji
Muktasari:
Mbunge wa Mbarali mkoani Mbeya (CCM), Haroon Pirmohamed ametoa msaada wa trekta ndogo za mkono (Powertiller) 102 zenye thamani ya zaidi ya Sh500 milioni ambazo zitagawanywa kwa vijiji vya jimbo hilo.
Mbarali. Mbunge wa Mbarali mkoani Mbeya (CCM), Haroon Pirmohamed ametoa msaada wa trekta ndogo za mkono (Powertiller) 102 zenye thamani ya zaidi ya Sh500 milioni ambazo zitagawanywa kwa vijiji vya jimbo hilo.
Mbunge huyo alikabidhi trekita kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla na viongozi wa vijiji 102 vya wilaya hiyo ambao walikabidhiwa na kuondoka nazo.
Pirmohamed alisema wananchi wa jimbo lake ambao wanategemea kilimo wanakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo moja ya utatuzi wa changamoto hizo ni trekta hizo hizo kwa kila kijiji ili waweze kuendeshea shughuli zao za kilimo na ujenzi.
“Mimi ni mkulima haswa na wananchi wangu wanategemea kilimo katika uzalishaji wao na wakabiliwa na changamoto nyingi. Hivyo nimeona kwa kuanzia tu kila kijiji kipatiwe trekta moja ili wazitumie kwenye maendeleo yao.
Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Mbarali, Yobu Mlomo alimueleza Makalla kwamba
msaada huo utafanya wilaya hiyo kuwa na ongezeko la trekta kutoka 2,394 hadi 2,496 ambazo zimesajiliwa.