Mbunge aungana na wenyeviti wa mitaa kumpinga DED

Muktasari:

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (DED) ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba aliagiza wenyeviti hao kurejesha mihuri ili ikabidhiwe kwa watendaji wa kata.

Mwanza. Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula ameungana na wenyeviti wa mitaa kupinga wasinyang’anywe mihuri.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (DED) ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba aliagiza wenyeviti hao kurejesha mihuri ili ikabidhiwe kwa watendaji wa kata.

Oktoba 22, wenyeviti wa mitaa 172 walisusia kikao kati yao na mkurugenzi huyo wakidai hawamtambui  kutokana na agizo lake la kuwataka kurejesha mihuri na kuikabidhi kwa watendaji wa kata.