Mchungaji Rwakatare awalipia faini wafungwa 43

Askofu  wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B,  Getrude  Rwakatare

Muktasari:

Akizungumza na  waandishi wa habari leo (Jumatano), Mchungaji  Rwakatare amesema hatua hiyo inalenga kuwasaidia watu hao waweza kuungana na familia zao, akiamini kwamba wamejutia makosa yao.

Dar es Salaam. Mchungaji  wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B,  Dk Getrude  Rwakatare amejitolea kuwalipia faini wafungwa 43 walioko kwenye Magereza mkoani Dodoma, wakiwamo wanaonyonyesha, wazee na wagonjwa.

Akizungumza na  waandishi wa habari leo (Jumatano), Mchungaji  Rwakatare amesema hatua hiyo inalenga kuwasaidia watu hao waweza kuungana na familia zao, akiamini kwamba wamejutia makosa yao.

"Wafungwa hao walihukumiwa kulipa faini labda Sh 50,000 au kiwango kingine kulingana na makosa na sheria inavyoeleza au kufungwa, kwa kuwa walikosa fedha wakafungwa jela, ambapo huko wamesababisha msongamano sasa kanisa limewalipia faini zao za jumla ni Sh6.8 milioni,” amesema.

Amesema wafungwa hao wamelipiwa faini bila kujali dini zao.

Habari zinazohusiana