Mdee amuangukia Ndugai -VIDEO

Muktasari:

  • Wengi wanamuona Mdee kama mtu asiyeogopa na ambaye hawezi kutetereshwa au kuyumbishwa na ambaye yuko tayari kuadhibiwa kwa kile alichokifanya.
  • Mara kadhaa ameadhibiwa au kutakiwa kufuta kauli, lakini hakuonekana kujali na wakati mwingine kutojutia kauli yake na badala yake kusema “ujumbe umefika”.

Dodoma. Wengi wanaomfahamu Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chadema, Halima Mdee wasingeamini macho yao kumuona juzi akijishusha na kunyenyekea.

Wengi wanamuona Mdee kama mtu asiyeogopa na ambaye hawezi kutetereshwa au kuyumbishwa na ambaye yuko tayari kuadhibiwa kwa kile alichokifanya.

Mara kadhaa ameadhibiwa au kutakiwa kufuta kauli, lakini hakuonekana kujali na wakati mwingine kutojutia kauli yake na badala yake kusema “ujumbe umefika”.

Lakini juzi jioni alionyesha upande wake wa pili; aliamua kuomba radhi kwa kosa alilofanya dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla, wabunge na wananchi wa Jimbo la Kawe na Watanzania kwa ujumla.

Inawezekana kuwa alilazimika kuomba radhi, lakini kauli zake zilionyesha kuwa alikuwa akijutia kosa lake.

“Mwenyekiti tarehe nne mwezi wa nne wakati wa uchaguzi wa Eala (wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki), kuna matukio ambayo yalitokea yakanipelekea kuzungumza lugha ambayo kitamaduni za Bunge sio sawa,” alisema Mdee kwa kuweka vituo virefu.

Habari Zinazohusiana