Meya Ilala azuia wamachinga kuondolewa katikati ya jiji

Meya wa Ilala, Charles Kuyeko akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar. Picha na Salim Shao

Muktasari:

Kauli ya Kuyeko imekuja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene kuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaondoa machinga maeneo ya katikati ya jiji.

Dar es Salaam. Meya wa Ilala, Charles Kuyeko amesema wamachinga waendelee kufanya biashara mjini na wasibughudhiwe na mtu yoyote.

Kauli ya Kuyeko imekuja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene kuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaondoa machinga maeneo ya katikati ya jiji.

Hivi karibuni alipokuwa Mwanza, Rais John Magufuli aliruhusu wafanyabiashara hao waendelee kufanya kazi kati kati ya mji hivyo hata wa jijini hapa wanaguswa na kauli hiyo.