Meya Ubungo atuma rambirambi Uingereza

Muktasari:

Tukio hilo lilitokea Juni 13 mwaka huu na Kamanda wa Polisi, Stuart Cundy  alisema idadi ya watu 58  wanakadiriwa kufariki dunia  katika jengo hilo lililokuwa na watu wapatao 600.

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema halmashauri yake inaungana na Manispaa ya London, Uingereza kuomboleza vifo vilivyotokea katika tukio la moto kwenye Jengo la Grenfell Tower.

Tukio hilo lilitokea Juni 13 mwaka huu na Kamanda wa Polisi, Stuart Cundy  alisema idadi ya watu 58  wanakadiriwa kufariki dunia  katika jengo hilo lililokuwa na watu wapatao 600.

Jacob ambaye pia ni diwani wa Ubungo (Chadema), alisema hayo jana wakati wa salamu zake kwa Meya wa London, Sadiq Aman Khan alizoziwasilisha kupitia kwa Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke.

Kwa niaba ya Manispaa ya Ubungo, natuma salamu za rambirambi  kwa Balozi wa Uingereza ambaye atafikisha ujumbe huo kwa meya Khan.

“Tunawapa pole sana wafiwa na majeruhi na famila zilizofikwa na janga hili,” alisema Jacob ambaye pia ni Mjumbe Kamati Kuu ya Chadema.

Katika salamu hizo, Jacob alisisitiza kuwa Manispaa ya Ubungo inaungana na Uingereza kwa ajili ya kuombeleza vifo hivyo na kumuomba Mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu sanjari na kuwaombea majeruhi wapate ahueni haraka.