Mfumo wa elimu watakiwa kuangaliwa upya

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez .

Muktasari:

  • Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Dk Natalia Kanem.

Dar es Salaam.  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amesema ili kukabiliana na tatizo la ajira, kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko katika mfumo wa utoaji elimu hapa nchini.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Dk Natalia Kanem.

Dk Kanem ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon kuwa Katibu Mkuu Msaidizi na Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia mipango katika Shirika la Umoja w