Mgeja amjia juu Polepole

Muktasari:

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hampyrey Polepole aache mara moja kugeuza

Morogoro. Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja amemuonya

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hampyrey Polepole aache mara moja kugeuza

matukio ya kuuawa Watanzania katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kuyageuza kama mtaji wa kisiasa kwa CCM ili CCM ionewe huruma na kuvichonganisha vyama vingine na wananchi.

Mgeja alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa mkoani

Morogoro akitokea Dar-s-Salaam.

Mgeja alisema kila mpenda amani nchini amesikitishwa na kauli yenye

ukakasi alizotoa Polepole hivi karibuni akisema CCM inakemea na imekuwa ikikemea maafa

hayo lakini vyama vya upinzani vikikaa kimya.

Mwenyekiti huyo amemshangaa Polepole kwa maneno yake akimtaka

atambue kila Mtanzania mpenda amani kwa matukio yanayotokea wilayani

Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani yanawagusa moja kwa moja

bila kujali dini zao, ukabila wao wala vyama vyao vya siasa.

 

“Tumesikitishwa kwa kauli za Polepole za kwake bila kujali msingi na

wala siyo kipindi muafaka wakati taifa lina majonzi makubwa,"alisema.