Mgodi kilipotokea kifo tata wafungwa

Muktasari:

Ofisi ya madini mkoani Geita imeufunga mgodi wa dhahabu wa Nyamahuna uliopo Wilaya ya Geita kupisha uchunguzi, kufuatia kifo cha mfanyakazi wake.

Geita. Ofisi ya madini mkoani Geita imeufunga mgodi wa dhahabu wa Nyamahuna uliopo Wilaya ya Geita kupisha uchunguzi, kufuatia kifo cha mfanyakazi wake.

Kaimu ofisa madini mkoani hapa, Fabian Mshai amesema wameufunga kuchunguza tuhuma zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuwa raia wa China amempiga mfanyakazi wake na kumuua.

Tayari vyombo vya usalama vimeanza kuchunguza mgodi huo unaomilikiwa na Mtanzania, Edru Bolle.