Mgombea udiwani CCM apita bila kupingwa

Dokta Anatory Amani akipongezwa na baadhi ya wananchi baada ya kutangazwa kupita bila kupingwa uchaguzi wa diwani kata ya Kagondo

Muktasari:

Msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo, Veda Kyaishozi amemtangaza leo Septemba 22, 2018 na kumkabidhi barua kama diwani mteule wa kata hiyo

 

Bukoba. Mgombea udiwani wa CCM Kata ya Kagondo Dk Anatory Amani amepita bila kupingwa baada ya vyama vya upinzani kutokuweka mgombea udiwani kwenye kata hiyo.

Msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo, Veda Kyaishozi amemtangaza leo Septemba 22, 2018 na kumkabidhi barua kama diwani mteule wa kata hiyo.

Baada ya kukabidhiwa barua hiyo Dk Amani amesema

wanachama wa CCM walijiandaa kupambana kwa ajili yake ili kupata ushindi na kubainisha kuwa yupo tayari kuwatumikia.