Mhadhiri UDOM auawa kwa kuchomwa kisu na mumewe

Muktasari:

Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatriece Mtenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo


Dodoma.  Mhadhiri wa Chuo cha Biashara katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rose Mdenye ameuawa  kwa madai ya kuchomwa kisu na mumewe usiku wa kuamkia leo Mei 26.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo asubuhi, Ofisa Uhusiano wa Chuo hicho, Beatriece Mtenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Mtenga amesema msiba upo Kisasa Sheli.