Omog awaweka kitako wachezaji

Kocha wa Simba, Joseph Omog .

Muktasari:

Akizungumza na wachezaji hao jana, Mcameroon huyo alisema kwanza ni kuhakikisha wanapata ushindi kwa kutumia mfumo wa 4-2-3-1.

Morogoro. Kocha wa Simba, Joseph Omog amewakalisha chini wachezaji wake na kuweka mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri msimu ujao.

Akizungumza na wachezaji hao jana, Mcameroon huyo alisema kwanza ni kuhakikisha wanapata ushindi kwa kutumia mfumo wa 4-2-3-1.

Jambo la pili, Omog aliwataka wachezaji kufahamu katika kikosi chake hakuna nyota zaidi ya Simba, kwa wale wanaojifanya wao ni zaidi ya timu hawana nafasi katika kikosi chake.

 “Jumapili ilikuwa maalumu na mwanzo wetu wa ngwe nyingine ya maandalizi, kuanzia Jumatatu kwa sababu kuna mambo yatabadilika katika mazoezi yetu  na sasa tutafanya ufundi zaidi na utimamu wa mwili itakuwa kidogo. Tulipoanza ilikuwa ni kuweka mwili sawa zaidi na ufundi kidogo,” alisema Omog.