Sunday, March 19, 2017

Barie aahidi medali Mbio za Nyika

By Imani Makongoro

Kocha wa timu ya riadha ya Tanzania inayojiandaa na Mbio za Dunia za Nyika, Zacharia Barie ametoa matumaini ya  Tanzania kushinda medali za dunia kwenye mashindano ya mbio za Nyika yatakayofanyika Jumapili ijayo nchini Uganda.

Barie, mwanariadha aliyewahi kuipa heshima Tanzania katika mbio mbalimbali za kimataifa, amesisitiza kuwa vijana wake hawatatoka patupu baada ya mbio hizo za vikwazo zitakazoshindanisha nguli wa riadha duniani zaidi ya 500.

Kikosi cha Tanzania kitakabidhiwa bendera keshokutwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye kwa ajili ya safari ya Uganda Alhamisi. Mashindano ya riadha yatafanyika Machi 26 kwenye mji wa Kampala, Uganda.

"Kwanza ni uzalendo wa wanariadha tangu tulipoanza mchakato wa maandalizi vilevile maandalizi waliyofanya si ya kubahatisha ni maandalizi ya ushindani," amesema na kuongeza.

-->