Danilo aeleza alivyowatosa Chelsea

Muktasari:

  • Danilo alikuwa akiwndwa pia na Chelsea, lakini beki huyo wa kulia aliamua kwenda kuungana na Pep Guardiola huko Man City kwa ada ya uhamisho ya Pauni 26.9 milioni.

Beki Mbrazili, Danilo amesema wala hakikuwa kitu kigumu kuichagua Manchester City mbele ya Chelsea wakati alipoamua kuihama Real Madrid katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Danilo alikuwa akiwndwa pia na Chelsea, lakini beki huyo wa kulia aliamua kwenda kuungana na Pep Guardiola huko Man City kwa ada ya uhamisho ya Pauni 26.9 milioni.